WAANDAMANAJI WACHOMA MAGARI MOMBASA
Kundi moja la waandamanaji jijini Mombasa limeteketeza takribani magari matano wakati wa maandamano huku wakiimba nyimbo za kumtaka rais William Ruto aondoke mamlakani.
Hata hivyo, kikosi cha wazima moto kimewasili na kuanzisha juhudi za kuzima moto huo, huku kiini cha kuteketeza magari hayo ikiwa bado hakijulikani..
Maandamano yameendelea katika maeneo kadhaa ya Mombasa, ikiwemo Mwembe Tayari na kituo kikuu cha magari ya uchukuzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































