DCI INACHUNGUZA MADAI YA UUZAJI WA SILAHA ILIYOMUUA TOM MBOYA
Idara ya Upelelezi dci inasema imeanza uchunguzi baada ya ripoti kuibuka kuwa mzee wa miaka 92 anadaiwa kununua bastola ambayo ilitumika kumuua Tom Mboya.
Katika chapisho kwenye X, DCI imesema hatua itachukuliwa uchunguzi utakapokamilika
Mboya aliuawa kwa kupigwa risasi Julai 5, 1969, katika Barabara ya Moi Avenue.
Habari za kuuawa kwa Mboya zilienea kama moto wa nyika na kusababisha ghasia jijini huku Wakenya wakimiminika kwa wingi katika Hospitali ya Nairobi kushuhudia kifo chake huku maafisa wa polisi wakilazimika wakati huo kuingilia kati kudhibiti umati wa watu.
Kizaazaa zaidi kilifuata wiki moja baadaye wakati wa misa ya mahitaji ya Mboya wakati waandamanaji wenye hasira walipambana na polisi tena.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































