WAKAZI WA LITEIN WALALAMIKIA UHALIFU NA UKOSEFU WA MIUNDOMBINU
Baadhi ya wakazi wa Litein, Kaunti ya Kericho, wameitaka serikali ya kaunti kuingilia kati na kushughulikia ongezeko la visa vya uhalifu na hali duni ya miundombinu.
Kulingana na wakazi eneo hilo halina taa za barabarani, jambo linalowafanya wafanyabiashara kuwa shabaha rahisi kwa wahalifu. Pia wamelalamikia ukosefu wa maji wa mara kwa mara, hali inayovuruga shughuli zao za kila siku na biashara.
Wakazi hao wametishia kuandamana endapo hatua haitachukuliwa kushughulikia malalamiko yao.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































