#uncategorized

SERIKALI KUANZISHA MFUMO WA MIUNDOMBINU JULAI

Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi amesema Mfuko wa Kitaifa wa Miundombinu utaanza kufanya kazi rasmi mwezi Julai mwaka huu kusaidia kufadhili miradi ya maendeleo nchini.

Mbadi akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu kawi amesema baadhi ya miradi ya nishati imewekwa chini ya mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi.

Aidha amesema baadhi ya miradi imehamishiwa chini ya Mfuko wa Kitaifa wa Miundombinu ili kuimarisha utekelezaji wake na kupunguza utegemezi wa mikopo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *