MARAGA AKOSOA SERIKALI KWA KUPUUZA MAAGIZO YA MAHAKAMA
Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga ameikosoa serikali kwa kupuuza maagizo ya mahakama na kuahidi kulinda utawala wa sheria iwapo atachaguliwa kuwa rais.
Akizungumza katika kaunti ya Turkana Cwakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ukombozi, Maraga amesema serikali ya sasa haiheshimu Katiba wala maamuzi ya mahakama.
Amedai kuwa serikali imekuwa ikipuuzilia mbali maagizo ya fidia kwa wananchi waliojeruhiwa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama wakati wa maandamano.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































