#Local News

RUTO ATAKA MAGEUZI YA HARAKA KATIKA UMOJA WA AFRIKA

Rais William Ruto ametaka kuharakishwa kwa mageuzi ndani ya Umoja wa Afrika ili bara la Afrika liweze kujitegemea zaidi kupitia taasisi imara na ufadhili endelevu.

Rais amesema Afrika lazima ipunguze utegemezi wa nje na kuimarisha uwezo wake wa kushughulikia changamoto zake kupitia utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

Ruto amezungumza baada ya kuongoza kikao cha nne cha kamati maalum ya wakuu wa nchi kuhusu mageuzi ya Umoja wa Afrika kilichofanyika kwa njia ya mtandao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *