#Local News

STEPHEN MULE AKOSOA MFUMO WA UAGIZAJI MAFUTA

Mbunge wa Matungulu Stephen Mule amekosoa mfumo wa serikali kwa serikali wa uagizaji wa mafuta akitaka soko huria lirejeshwe.

Mule pia amependekeza kupunguzwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa mafuta kutoka asilimia 8 hadi 4 ili kupunguza mzigo kwa wananchi.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja humu nchiniMule amesema mfumo wa sasa umepunguza ushindani na kuchangia kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *