#Local News

UPINZANI WASHINIKIZA MAJIBU KUHUSU KIFO CHA JIRONGO

Upasuaji wa maiti ya aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo unatarajiwa kufanywa leo ili kubaini chanzo cha kifo chake, huku idara ya upelelezi nayo ikianzisha uchunguzi katika ajali inayoripotiwa kumwangamiza mbunge huyo wa zamani.

Maafisa wa idara hiyo wanachunguza kanda za video za CCTV kutoka kituo cha mafuta kwenye barabara ya Nairobi-Nakuru alikoingia kabla ya kuanza safari ya kurejea Nairobi majira ya saa nane usiku na kisha kuhusika kwenye ajali dakika chache baadaye.

Viongozi wa upinzani wameibua maswali, ikiwemo hali ya abiria waliokuwa kwenye basi lililogongana na gari la Jirongo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UPINZANI WASHINIKIZA MAJIBU KUHUSU KIFO CHA JIRONGO

POLISI WACHUNGUZA VILIPUZI NYATIKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *