#Athletics #Sports

VIPIMA UBORA WA HEWA VYAWEKWA KABLA YA MBIO ZA NAIROBI CITY MARATHON

Vipima ubora vya hewa vinne vimewekwa katika maeneo muhimu kando ya Barabara ya Nairobi Expressway kuelekea mashindano ya Nairobi City Marathon yatakayofanyika Juni 7.

Mashindano hayo yataanza City Hall Way na kumalizikia Uhuru Park huku sehemu kubwa ya mbio ikifanyika kwenye barabara hiyo.

Mtafiti wa masuala ya ubora wa hewa kutoka Taasisi ya Mazingira ya Stockholm Ngongang Wandji amesema vifaa hivyo vitasaidia kufuatilia kiwango cha uchafuzi wa hewa kabla, wakati na baada ya mashindano ili kuhakikisha mazingira salama kwa wanariadha.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *