#Football #Sports

MANCHESTER UNITED WANAPANGA KUMBAKISHA BRUNO FERNANDES

Manchester United wameanza mazungumzo ya kumbakisha nahodha wao Bruno Fernandes licha ya kuwepo kwa kipengele cha kuvunja mkataba wake chenye thamani ya pauni milioni 57.

Ripoti zinaeleza kuwa mazungumzo ya awali tayari yamefanyika huku klabu hiyo ikiwa tayari kumzawadi kiungo huyo kwa mkataba bora zaidi.

Bruno pia anaripotiwa kuvutiwa na vilabu vya Ulaya pamoja na Saudi Arabia, lakini Manchester United wanasisitiza kuwa wanamtaka aendelee kusalia Old Trafford.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *