CHELSEA WALAUMIWA KWA UTOVU WA NIDHAMU
Kocha wa muda wa Chelsea Calum McFarlane amesema utovu wa nidhamu ulikuwa sababu kubwa iliyosababisha timu hiyo kukosa nafasi ya kushiriki mashindano ya Ulaya msimu ujao.
Chelsea walimaliza katika nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufungwa mabao 2-1 na Sunderland Katika mechi ambayo, beki wa Ufaransa Wesley Fofana alitolewa nje kwa kadi nyekundu, ikiwa ni kadi nyekundu ya nane kwa Chelsea katika ligi msimu huu.
McFarlane amesema suala hilo limekuwa tatizo kubwa kwa timu katika msimu uliokuwa na changamoto nyingi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































