WAKAAZI WA TRANSNZOIA WAMTAKA RUTO ATIMIZE AHADI ZAKE KWAO
Wakaazi wa kaunti ya Transnzoia wamemtaka rais William Ruto kutimiza ahadi alizotoa kwao wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2022.
Kwa mujibu wa wakaazi hao rais Ruto aliahidi kuwapa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa soko la Masinde Muliro Complex lililoko mjini Kitale na vile vile kuanzisha ujenzi wa nyumba za bei nafuu hasa baada ya kuweka jiwe la msingi katika sehemu ya shamba la magereza.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































