#Local News

WAKENYA WAONYWA KUHUSU MVUA KUBWA INAYOTARAJIWA

Idara ya utabiri wa hali ya anga imetangaza kuwa baadhi ya maeneo yatapata mvua kubwa kuanzia leo Mei 26 hadi tarehe moja Juni mwaka huu.

Katika taarifa idara hiyo imesema maeneo yatakayo pata mvu hiyo ni pamoja na Nairobi, Nyeri, Murang’a, Kiambu,  kaunti ya Kakamega, Bungoma, Nandi, Uasin Gishu na Trans Nzoia, kaunti nyingine ni Mombasa, Kilifi na kwale.

Wakenya wameshauriwa kuepuka kuvuka mito iliyojaa maji,kuendesha magari kwenye barabara zilizofurika huku wakazi wa nyanda za chini wakishauri kutafuta hifadhi  katika nyanda za juu  ili kuepuka kusombwa na maji ya mafuriko.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *