HATMA YA NYARIBO SENETI
Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo kwa mara ya 3 ndani ya miaka 3 atategemea bunge la seneti kumwokoa na kumrejesha mamlakani, baada ya kubanduliwa na wawakilishi wadi 23 kati ya 31 wa bunge la kaunti hiyo hapo jana.
Spika wa bunge hilo Thaddeus Nyabaro, anatarajiwa kulifahamisha bunge la seneti kuhusu kubanduliwa huko kabla ya seneti kutenga siku ya kusikiliza hoja hiyo na kudumisha au kubatilisha uamuzi wa wawakilishi wadi hao.
Nyaribo anatuhumiwa kwa utumiaji mbaya wa afisi na ukiukaji wa sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































