#Local News

MBADI APUUZA SIASA, AELEKEZA MACHO MAENDELEO

Waziri wa Fedha John Mbadi amepuuzilia mbali mjadala kuhusu mustakabali wake wa kisiasa huku taifa likielekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, akisema hilo si jambo linalomsumbua kwa sasa.

Mbadi amsema kipaumbele chake ni kujenga Kenya yenye maendeleo na kuhakikisha sera za kiuchumi zinawanufaisha wananchi, badala ya kujihusisha na siasa za kujilinda kazini baada ya uchaguzi.

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa ushirikishwaji wa umma kuhusu Bajeti na Ubinafsishaji uliofanyika katika Chuo cha Kitaifa cha Kiambu Polytechnic.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *