KRA YAPENDEKEZA USAJILI WA LAZIMA WA VAT KWA BIASHARA ZOTE
Mamlaka ya kukusanya Ushuru nchini (KRA) imependekeza mageuzi makubwa ya ushuru ambayo yatafanya kuwa lazima kwa biashara zote, bila kujali ukubwa, kusajiliwa kama mawakala wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Hatua hiyo, ikiwa itapitishwa, itaondoa kiwango cha sasa cha mauzo ya kila mwaka cha Ksh5 milioni kwa usajili wa VAT, na kuwafanya wafanyabiashara wadogo wadogo kulipa ushuru kwa mara ya kwanza. Chini ya pendekezo hilo, kila biashara, kuanzia maduka ya reja reja na watoa huduma hadi washauri, italazimika kutoza asilimia 16 ya VAT kwa bidhaa na huduma ambazo hazijaondolewa ushuru na baadaye makusanyo hayo kupelekwa kila mwezi kwa KRA.
Hii ina maana wafanyabiashara wadogo ambao hapo awali walifanya kazi chini ya kiwango cha VAT, ikiwa ni pamoja na maduka ya kuuza simu za mkononi, vinywaji, maji ya chupa, gesi ya kupikia, vipodozi na bidhaa za petroli, sasa watalazimika kujumuisha VAT katika bei zao.Hata hivyo, hii inaweza kutafsiri katika kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma za kila siku na kulazimu wafanyabiashara wadogo kurekebisha miundo yao ya bei ili kukidhi VAT ya asilimia 16.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































