WAKENYA WAONYWA KUHUSU MVUA KUBWA INAYOTARAJIWA
Idara ya utabiri wa hali ya anga imetangaza kuwa baadhi ya maeneo yatapata mvua kubwa kuanzia leo Mei 26 hadi tarehe moja Juni mwaka huu.
Katika taarifa idara hiyo imesema maeneo yatakayo pata mvu hiyo ni pamoja na Nairobi, Nyeri, Murang’a, Kiambu, kaunti ya Kakamega, Bungoma, Nandi, Uasin Gishu na Trans Nzoia, kaunti nyingine ni Mombasa, Kilifi na kwale.
Wakenya wameshauriwa kuepuka kuvuka mito iliyojaa maji,kuendesha magari kwenye barabara zilizofurika huku wakazi wa nyanda za chini wakishauri kutafuta hifadhi katika nyanda za juu ili kuepuka kusombwa na maji ya mafuriko.
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































