LUSAKA AONYA WAFANYAKAZI HEWA KAUNTI YA BUNGOMA
Gavana wa Bungoma Ken Lusaka ameagiza bodi ya uwajiri katika kaunti hiyo kuangazia kwa kina swala la wafanyakazi hewa kuripotiwa katika utumishi wake akisema kuna wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao hawakuidhinishwa kisheria.
Lusaka ameagiza uchunguzi kufanywa kuhusu jinsi wafanyakazi hao walivyoajiriwa akisema bodi hiyo inafaa kukaguliwa upya.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































