STARLETS YAJIANDAA KWA MECHI DHIDI YA UGANDA
Beki wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 Pauline Namisi pamoja na mshambuliaji Emily Adhiambo wamesema timu hiyo itategemea ukomavu, nidhamu ya kiufundi na sapoti ya mashabiki katika mechi ya marudiano dhidi ya Uganda.
Wachezaji hao wameeleza kuwa sare ya mabao 1-1 waliyoipata katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa FUFA Stadium imewapa somo muhimu kabla ya pambano la marudiano litakalochezwa Jumapili katika uwanja wa Nyayo.
Namisi amesema Uganda walikuwa na dhamira ya kushinda nyumbani lakini Kenya ilionyesha uimara mkubwa chini ya presha na kufanikiwa kuweka ushindani wazi kuelekea mechi ya Nairobi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































