RUTO: WALIO NA MISHAHARA YA CHINI YA SH30,000 WASILIPISHWE KODI
Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itapeleka bungeni pendekezo la kuwaondoa wafanyakazi wanaopata mshahara wa hadi shilingi elfu 30 katika ulipaji wa kodi ya mapato.
Akizungumza katika kikao cha Kitaifa cha Maombi jijini Nairobi, Ruto amesema hatua hiyo inalenga kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wa kipato cha chini licha ya serikali kukabiliwa na upungufu wa mapato wa takriban shilingi bilioni 40.
Rais pia amesema serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 28 katika miezi miwili iliyopita kudhibiti ongezeko la bei ya mafuta na kupunguza mzigo kwa wananchi pamoja na sekta ya uchukuzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































