#uncategorized

HUZUNI GILGIL BAADA YA MOTO WA SHULE, DNA KUFANYWA

Maumivu na simanzi vilitawala katika shule ya Utumishi Girls Academy eneo la Gilgil huku wazazi na walezi wakihangaika kutafuta taarifa za watoto wao kufuatia moto uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine 79.

Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura amesema mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor tayari amewasili eneo hilo kuanza uchunguzi wa vinasaba vya DNA ili kusaidia kutambua miili ya waliofariki kabla ya kukabidhiwa familia zao.

Mwaura ameahidi kuwa serikali itaendelea kutoa msaada kwa familia zilizoathirika huku wazazi wengi wakionekana kugubikwa na huzuni na majonzi kufuatia mkasa huo mkubwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *