ANTHONY GORDON AELEKEA BARCELONA KWA ADA KUBWA
Anthony Gordon yuko mbioni kujiunga na FC Barcelona baada ya bodi ya Newcastle United pamoja na wamiliki wao kutoka Saudi Arabia kukubali ofa rasmi ya uhamisho huo.
Taarifa zinaeleza kuwa Barcelona italipa euro milioni 70 pamoja na nyongeza mbalimbali zitakazofikisha thamani ya dili hilo zaidi ya euro milioni 80 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.
Gordon anatarajiwa kusafiri wiki hii kwenda Hispania kwa uchunguzi wa afya na kusaini mkataba rasmi, hatua inayotarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ya Catalonia kuelekea msimu mpya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































