#Local News

FAMILIA KIBRA YATAKA HAKI BAADA YA MWANAMKE KUCHOMWA MOTO KIBRA

Familia moja katika eneo la Gatwikira huko kibra inataka haki baada ya ndugu yao kudaiwa kushambuliwa kutokana na msimamo wake wa kisiasa.

Maureen Matsili ambaye ni mama wa watoto wanne, anadaiwa kushambuliwa na kuchomwa moto Mei 18 na mtu anayemfahamu kutokana na kuunga mkono kauli mbiu ya “Two Term” katika eneo hilo.

Polisi wa Kibra wanaendelea kuchunguza tukio hilo kama uhalifu unaohusishwa na chuki huku familia ikitaka mshukiwa akamatwe na kufikishwa mahakamani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *