#uncategorized

MAHAKAMA YASITISHA MPANGO WA KITUO CHA EBOLA

Mahakama Kuu imesitisha kwa muda mpango wa serikali wa kuanzisha au kuendesha kituo chochote cha karantini, kutenga au kutibu Ebola nchini Kenya chini ya makubaliano yoyote na Marekani au serikali nyingine za kigeni.

Mahakama pia imezuia serikali kuwaruhusu kuingia nchini, kuwapokea au kuwahamisha watu waliothibitishwa au wanaoshukiwa kuathiriwa na virusi vya Ebola hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Amri hizo zilitolewa baada ya Mahakama kuthibitisha kuwa ombi lililowasilishwa na Katiba Institute ni la dharura, huku kesi hiyo ikipinga madai ya makubaliano kati ya Kenya na serikali za kigeni kuhusu usimamizi wa visa vya Ebola.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *