RAIA WA MAREKANI WALIOAMBUKIZWA EBOLA WATARAJIWA KUPATA MATIBABU NCHINI
Huku kenya ikiendelea kulinda mipaka zake dhidi ya kusambaa kwa virusi vya Ebola Rais wa marekani Donald Trump anasema kwamba raia wa marekani walioambukizwa virusi vya Ebola nchini Demokrasia ya Congo DRC sasa wataletwa hapa nchini Kenya kwa uangalizi wa matibabu badala ya kurudishwa badala ya kurejeshwa huko marekani.
Kulingana na gazeti rasmi la marekani serikali ya taifa hilo inapanga kuanzisha kituo muhimu humu nchini kitakacho tumika kuwaweka karantini na kuwahudumia raia wake wanaoshukiwa kuambukizwa ugonjwa huo na maafisa wa matibabu watakao kuja nchini kutoka marekani baada ya kupewa mafunzo maalum.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































