#Football #Sports

ANN ALUOCH ASIFIA MAFANIKIO YA MATHARE UNITED WOMEN

Kocha wa Timu ya wanawake ya  Mathare United Ann Aluoch amesema mwanzo mzuri wa msimu, juhudi za wachezaji pamoja na usaidizi wa uongozi wa klabu vilichangia mafanikio ya timu hiyo katika Ligi ya Taifa ya Daraja la Kwanza kwa wanawake.

Mathare United walitwaa ubingwa wa Kanda A na kufuzu kushiriki ligi kuu baada ya kucheza mechi 21 wakipoteza mchezo mmoja pekee na kutoka sare mara moja.

Aluoch amesema timu iliingia msimu huu ikiwa na dhamira ya kurekebisha makosa ya msimu uliopita huku akiwapongeza wachezaji kwa kujitolea kwao katika safari ya kupanda daraja.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *