#Local News

DUALE: SHERIA ZA KENYA LAZIMA ZIHESHIMIWE KATIKA USHIRIKIANO WA EBOLA

Waziri wa Afya Aden Duale amesema makubaliano yoyote kati ya Kenya na mataifa ya kigeni kuhusu kushughulikia watu walioathiriwa na virusi vya Ebola lazima yaheshimu sheria za Kenya pamoja na kanuni za afya ya umma.

Kauli hiyo inajiri kufuatia ripoti kuwa Marekani inaweza kuzingatia kuwaleta nchini Kenya baadhi ya raia wake waliokaribiana na wagonjwa wa Ebola kwa uchunguzi au matibabu, jambo lililozua wasiwasi kuhusu uwezo wa taifa kukabiliana na hatari hiyo ya kiafya.

Duale amesisitiza kuwa mamlaka ya Kenya, taratibu za uhamiaji pamoja na hatua za usalama wa afya haziwezi kupuuzwa chini ya mfumo wowote wa ushirikiano wa kimataifa, akihakikishia wananchi kuwa serikali itaweka mbele usalama wa afya ya umma nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *