#Local News

WAZIRI OGAMBA AZUNGUMZA KATIKA ENEO LA MKASA  WA MOTO HUKO GILGIL

Waziri wa elimu Julius Ogamba amesema kati ya wanafunzi 808 ambao walikua  katika shule ya  wasichana ya Utumishi huko Nakuru  wakati wa mkasa wa moto wanafunzi 79 wamejeruhiwa, huku 71 wakihudumiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini, saba wakiendelea kupokea matibabu.

Akizungumza katika shule ya wasichana ya Utumishi Ogamba ametuma rambi rambi zake kwa familia na marafiki wa wale wanafunzi 16 ambao wameaga dunia kutokana na mkasa huo wa moto  akiahidi kuwa wizara yake itaikagua shule hiyo kubaini iwapo ilifuata muongozo wa usalama ambao ni sharti kwa shule za mabweni kufuatwa akisema ripoti hiyo itakapokamilika itawekwa wazi kwa umma.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *