MASWALI YAIBUKA KUHUSU MOTO WA SHULE YA UTUMISHI
Maswali yanaendelea kuibuka kuhusu chanzo cha moto ulioteketeza bweni katika shule ya Utumishi Girls Academy iliyoko Kaunti ya Nakuru huku Wakenya wengi wakieleza hofu kuhusu usalama wa wanafunzi katika mabweni ya shule.
Taarifa mpya zinaashiria kuwa huenda moto huo uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine 79 uliwashwa kimakusudi, jambo ambalo limeongeza wasiwasi miongoni mwa wananchi.
Viongozi pamoja na maafisa wa usalama waliotembelea shule hiyo wamesema uchunguzi wa kina umeanzishwa ili kubaini chanzo halisi cha mkasa huo huku wito ukitolewa kuimarisha viwango vya usalama katika shule za bweni nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































