WANDAYI AHAKIKISHIA NCHI KUHUSU UPATIKANAJI WA MAFUTA
Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi amesema Kenya ina akiba ya kutosha ya mafuta licha ya ripoti za uhaba katika baadhi ya maeneo ya ukanda huu kutokana na vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.
Wandayi ambaye alikagua vituo vya mafuta katika kaunti za Nairobi na Machakos amesema serikali imejitolea kuhakikisha usambazaji wa mafuta haukatizwi.
Aidha amewataka wananchi kuwa watulivu akisema bei ya mafuta inaweza kushuka mara hali ya soko la kimataifa itakapotengemaa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































