#uncategorized

MOTO WAZUKA SHULE YA GACHARAGE MURANG’A

Moto ulizuka usiku wa Alhamisi katika shule ya upili ya Gacharage eneo la Kandara Ruchu Kaunti ya Murang’a na kuzua hofu mpya kuhusu usalama wa taasisi za elimu nchini.

Tukio hilo limejiri saa chache baada ya mkasa wa moto katika shule ya Utumishi Girls Academy eneo la Gilgil uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine wengi kabla ya shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana.

Gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata amesema hakuna aliyepoteza maisha katika tukio hilo huku vikosi vya dharura vya kaunti vikipelekwa haraka kudhibiti moto huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *