#uncategorized

WATAALAMU WA EBOLA WA AMERIKA WAWASILI KENYA

Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka Amerika wamewasili nchini Kenya na kuanza maandalizi ya kituo maalum cha Ebola ambacho Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio amesema kitaanza kufanya kazi ndani ya siku saba zijazo.

Ikulu ya White House imethibitisha kuwa Amerika inaandaa kituo maalum nchini Kenya kwa ajili ya kuwatenga raia wa Marekani walioathiriwa au waliokaribiana na virusi vya Ebola, huku ikielezwa kuwa kituo hicho kitaendeshwa na kuhudumiwa kikamilifu na Wamarekani.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kituo hicho kinajengwa karibu na maeneo ya kijeshi ya Uingereza katika Kaunti ya Laikipia huku Rais William Ruto akiitisha kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri kujadili hali ya Ebola katika ukanda huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *