BUNGE LAHOJI BAJETI YA 2026/27
Wanachama wa Kamati ya Bajeti na Matumizi ya Fedha wameibua wasiwasi kuhusu upungufu wa mapato, uwajibikaji katika sekta ya afya pamoja na shinikizo la kifedha wakati wa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27.
Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi ametetea bajeti ya shilingi trilioni 4.785 yenye nakisi ya shilingi trilioni 1.111 itakayofadhiliwa hasa kupitia ukopaji wa ndani.
Hata hivyo wabunge wamehoji uhalisia wa makadirio hayo wakitaja ukusanyaji duni wa mapato pamoja na ukosefu wa ufafanuzi kuhusu mapato yanayokusanywa na serikali za kaunti.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































