DCI YAMKAMATA MUSHUKIWA WA MATAMSHI YA UCHOCHEZI MITANDAONI
Maafisa wa upelelezi wa kesi za jinai DCI wamemkamata mshukiwa anaehusishwa na matamshi ya uchochezi yaliyokuwa yakisambaa mitandaoni.
Katika taarifa DCI imesema Evans Onyango Kawala maarufu kama Kidero Jasuba amekamatwa katika eneo la Shujaa Mall mtaani Kayole jijini Nairobi.
Kulingana na DCI mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 33 anaendelea kuzuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani hapo kesho.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































