#Sports

JULIUS YEGO ATAKA MASHINDANO ZAIDI YA KIMATAIFA NCHINI

Bingwa wa zamani wa dunia wa mkuki Julius Yego ametaka shirikisho la riadha nchini AK kuandaa mashindano zaidi yaliyoidhinishwa na shirikishi la riadha duniani humu nchini ili kuwasaidia wanariadha kufuzu kwa urahisi mashindano ya dunia ya mwaka 2027 yatakayofanyika Beijing.

Kauli yake imejiri baada ya shirikisho la riadha duniani kutangaza viwango vipya vya kufuzu kwa mashindano hayo, ambapo wanariadha watalazimika kufikia viwango vilivyowekwa au kufuzu kupitia mfumo wa viwango vya ubora duniani.

Yego, ambaye alitwaa ubingwa wa dunia mwaka 2015, amesema masharti ya kufuzu yamekuwa magumu zaidi kadri miaka inavyosonga hasa kwa michezo ya uga, akisisitiza kuwa mashindano mengi ya kiwango cha kimataifa nchini yatawapa wanariadha nafasi bora ya kujikusanyia alama na uzoefu mkubwa wa ushindani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *