#Local News

KINDIKI ASEMA UCHAGUZI 2027 UTAAMULIWA NA MAENDELEO

Naibu Rais Kithure Kindiki ametetea rekodi ya maendeleo ya serikali akisema uchaguzi mkuu ujao utaamuliwa na utendakazi pamoja na utoaji huduma badala ya siasa za maneno.

Akizungumza katika eneo Bunge la Msambweni, Kindiki amesema serikali ya Kenya Kwanza inalenga kubadilisha maisha ya wananchi kupitia miundombinu, umeme, masoko na uchumi wa baharini.

Amesisitiza kuwa Rais William Ruto atatafuta muhula wa pili kwa msingi wa maendeleo yaliyotekelezwa katika sekta za barabara, umeme, bandari na masoko.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *