WAMOTO AIPA KABRAS NAFASI YA KUTWAA ENTERPRISE CUP
Kocha wa raga wa Chuo Kikuu cha Kibabii Peter Wamoto ameipa Kabras RFC nafasi kubwa ya kutwaa taji la Enterprise Cup katika fainali itakayochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa RFUEA Grounds.
Kabras wanapania kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita mfululizo baada ya hivi karibuni kutwaa taji la Kenya Cup kwa mara ya tano mtawalia huku wakikabiliwa na klabu ya Stanbic Black Pirates kutoka Uganda.
Timu hiyo ya Kakamega ilifika fainali baada ya kuichapa Menengai Oilers alama 29-20 katika nusu fainali huku Black Pirates wakiiandika historia kwa kuwa klabu ya kwanza kutoka Uganda kufika fainali hiyo tangu mwaka 1970 baada ya kuiondoa Nondescript.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































