NJERI MAINA ATAKA HATUA ZA DHARURA DHIDI YA MAUAJI YA WANAWAKE
Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Kirinyaga Njeri Maina ametaka kuwepo kwa hatua za haraka na za pamoja kitaifa kukabiliana na ongezeko la mauaji ya wanawake na watoto wanaopotea nchini.
Katika taarifa yake, Maina amesema visa vinavyoongezeka vya wanawake kuuawa na watoto kutoweka vinaonyesha kuwa taifa linakabiliwa na janga kubwa linalohitaji ushirikiano wa taasisi zote za serikali pamoja na jamii.
Aidha amesema juhudi zilizopo kwa sasa bado hazijaratibiwa ipasavyo na mara nyingi huwa za kuitikia matukio badala ya kuzuia matatizo hayo mapema.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































