RUTO AZINDUA MPANGO WA KUPUNGUZA VIFO VYA KINA MAMA NA WATOTO WACHANGA
Rais William Ruto amezindua rasmi mpango wa kitaifa wa EWENE wa miaka 2026 hadi 2028 unaolenga kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga nchini.
Mpango huo unalenga kuboresha huduma za afya, kuimarisha uwajibikaji pamoja na kutekeleza afua maalum katika kaunti zinazorekodi visa vingi vya vifo vya kina mama na watoto wachanga.
Serikali pia imeanzisha mpango wa miezi sita wa matokeo ya haraka katika afya ya mama na mtoto utakaotekelezwa hadi Novemba mwaka 2026 ili kuharakisha utekelezaji wa huduma na kuboresha matokeo ya afya nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































