#Local News

UHABA WA MALAZI WAIBUKA WAJIR KABLA YA MADARAKA DEI

Mji wa Wajir unakabiliwa na uhaba mkubwa wa malazi kuelekea sherehe za kitaifa za Madaraka Day zitakazoongozwa na Rais William Ruto Jumatatu ijayo.

Maelfu ya wageni kutoka maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo wakiwemo viongozi wa kitaifa, maafisa wa usalama pamoja na wanamuziki.

Hoteli na nyumba nyingi za wageni mjini humo zimeripotiwa kujaa mapema huku baadhi ya wageni wakikosa maeneo ya malazi kutokana na idadi kubwa ya watu wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *