#Football #Sports

SWEDEN WATEGEMEA ISAK NA GYOKERES KATIKA KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Sweden inatarajia safu yao ya ushambuliaji ikiongozwa na Alexander Isak na Viktor Gyokeres kuwasaidia kufanya vyema katika Kundi F la Kombe la Dunia mwaka huu.

Timu hiyo chini ya kocha Graham Potter itachuana na Uholanzi, Japan pamoja na Tunisia nchini Marekani, Canada na Mexico.

Sweden walifika fainali hizo kwa njia ngumu baada ya kukusanya pointi mbili pekee katika mechi sita za kufuzu na kumaliza mkiani mwa kundi lao.

Lakini Baadaye walifuzu kupitia mchujo baada ya kumaliza nafasi bora katika mashindano ya Uefa Nations League.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *