#Local News

RAIS RUTO AHUDHURIA KIKAO CHA KITAIFA CHA MAOMBI

Rais William Ruto amewasili katika hoteli ya  Safari Park kuhudhuria hafla ya kikao cha Kitaifa cha Maombi kinachowaleta pamoja viongozi wa kisiasa, kidini na serikali

Viongozi mbalimbali wa kitaifa, wanasiasa pamoja na maafisa wa serikali pia wamewasili katika hafla hiyo inayolenga kuombea taifa na kuhimiza mshikamano wa kitaifa

Hafla hiyo ya kila mwaka huwakutanisha viongozi kutoka sekta tofauti nchini kwa maombi, tafakari na mijadala kuhusu masuala yanayohusu maendeleo, uongozi na umoja wa taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *