#Local News

UTAFITI WA KNUT WAFICHUA WALIMU WANAKABILIWA NA MADENI

Utafiti mpya wa Muungano wa KNUT umefichua kuwa walimu wengi nchini wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha, msongo wa mawazo na uchovu wa kazi.

Ripoti ya ustawi na ushiriki wa walimu imeonyesha kuwa asilimia 97 ya walimu wanaishi kutegemea mshahara wa mwezi bila kuwa na akiba yoyote mwishoni mwa mwezi.

Aidha, asilimia 92 ya walimu walioshiriki katika utafiti huo walisema wako hatarini kushindwa kukabiliana na gharama za dharura huku asilimia 88 wakisema wanapata ugumu kulipa madeni yao na wakati huo huo kudumisha maisha yao ya kawaida.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *