WAFANYABIASHARA WAACHWA NA HASARA
Wafanyabiashara katika maeneo hasa Nairobi, Meru, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Nakuru, Machakos na Kajiado wameendelea kukadiria hasara ya mamilioni ya pesa baada ya biashara zao kuporwa huku zingine zikiteketezwa na makundi ya wahundi waliotumia maandamano ya Saba Saba kutekeleza uhalifu.
Miongoni mwa taasisi za serikali zilizochomwa ni afisi ya NG-CDF ya Kirinyaga Central, idara ya polisi ikiripoti kuwa magari 15 ya serikali na 4 ya kibinafsi yaliharibiwa.
Uharibifu huo ulitokea licha ya hakikisho la polisi la kulinda Maisha na mali wakati wa maandamano hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































