UBASHIRI WAONYA KUHUSU MAFURIKO
Idara ya utabiri wa hali ya anga imewataka wakenya kutahadhari kuhusu uwezekano wa mafuriko kutokana na mvua inayoendelea katika maeneo mbali mbali ya nchi.
Kulingana na idara hiyo, huenda mvua inayoendelea ikaandamana na upepo mkali na ngurumo za radi, maeneo yaliyo katika nyanda za chini yakirataibiwa kuwa na mafuriko.
Wakenya wameshauriwa kutopita katika maji ya mafuriko iwe kwa miguu au kwa magari.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































