#Sports

KENYA YAJIONGEZEA MEDALI ANGOLA

Matineja wa Kenya wanaoshiriki michezo ya vijana wa Afrika mwaka huu nchini Angola wamevuna medali 6 zaidi na kufikisha jumla ya medali 23 katika michezo hiyo.

Ushindi wa medali hizo za jana ulianzishwa na mwanamichezo chipukizi wa kunyanyua vyuma Amanda Lina, aliyeshinda nishani 2 za fedha na shaba 1 katika katika vipengele vya snatch and clean and jerk, akifikia mafanikio adimu ya medali tatu katika uzani wa kilo 48.

Tineja huyo ameshuhudia kuimarika mchezoni, baada ya kutamalaki katika mashindano sawa ya mwaka jana jijini Nairobi ambapo alishinda nishani 6 za fedha.

Katika mchezo wa taekwondo, Rachel Wekesa mwenye umri wa miaka 15, alipata nishani ya fedha baada ya kugaragazwa na Leyan Yasser Mohammed wa Misri katika fainali za uzani wa kilo 48.

Kwenye pambano la wavulana, Gideon Robert aliishindia Kenya nishani ya shaba baada kupoteza dhidi ya Issaka Mahamadou wa Ivory Coast katika pambano la kusaka nafasi ya 3.

Aidha, Clinton Omondi aliyekuwa akishiriki kwa mara ya kwanza, aliishindia Kenya shaba katika pambano na masumbwi kwa wachezaji walio chini ya uzani wa kilo 50.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KENYA YAJIONGEZEA MEDALI ANGOLA

WAITITU, MKEWE MAHAKAMANI

KENYA YAJIONGEZEA MEDALI ANGOLA

POLICE FC WATIWA PINGU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *