#Local News

UCHUNGUZI WA DCI KUHUSU KIFO CHA JIRONGO

Aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo alifariki kwenye ajali ya kawaida na wala hakuna uhalifu uliohusika kutokana na ushahidi uliopo.

Haya ni kulingana na taarifa ya idara ya upelelezi DCI, ambayo imeripoti kuwahoji na kuandikisha taarifa kutoka kwa watu kadhaa akiwemo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, dereva wa basi la Climax Coaches Tiras Kamau na msaidizi wake, mmiliki wa mkahawa alikokuwa Jirongo kabla ya kifo chake, mbali na uchunguzi wa kanda za CCTV kutoka kituo cha petroli cha Eagols eneo la Naivasha.

DCI imeahidi kukamilisha uchunguzi na kuwasilisha faili kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma ili kutoa mwelekeo, huku akitaka umma na wanasiasa kukoma kueneza uvumi kuhusu kifo hicho.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UCHUNGUZI WA DCI KUHUSU KIFO CHA JIRONGO

WAZAZI NJIA PANDA KUHUSU GRADE 10

UCHUNGUZI WA DCI KUHUSU KIFO CHA JIRONGO

HOFU YA AJALI BARABARANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *