#Local News

WANNE WAFARIKI KWENYE JENGO SHAURI MOYO

Shughuli za uokoaji zinaendelea mtaani Shauri Moyo jijini Nairobi ambako jumba moja limeporomoka na kuwaua watu 4 huku wengine 4 wakiokolewa.

Kwa mujibu wa wizara ya usalama wa kitaifa, jumba hilo ni miongoni mwa mijengo inayoendelea kubomolewa na tume inayosimamia uimarishaji wa Nairobi River katika eneo la Blue Estate, karibu na mto huo.

Watu zaidi wanahofiwa kukwama kwenye jengo hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *