#Football #Sports

3K FC YAMTANGAZA OMASETE KUWA KOCHA MKUU

Klabu ya 3K FC inayoshiriki Ligi ya National Super League imemthibitisha Nicodemus Omasete kuwa kocha wake mkuu mpya baada ya kuonyesha kiwango bora alipokuwa kama kocha wa muda.

Omasete anachukua nafasi ya Francis Chege kufuatia kushuka kwa matokeo kulikosababisha mabadiliko katika benchi la ufundi.

Tangu achukue majukumu hayo, Omasete ameiongoza timu hiyo kushinda mechi sita mfululizo katika mashindano ya ligi na kombe, ikifunga mabao 22 na kuruhusu bao moja pekee

Akizungumza baada ya kuthibitishwa kwake, Omasete amesisitiza kuwa falsafa yake ya kushambulia imekuwa nguzo ya mafanikio ya timu hiyo, akibainisha kuwa mabao ya mapema yamechangia pakubwa ushindi wao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *