#Football #Sports

KARIOBANGI SHARKS WAKABILIWA NA MTIHANI MGUMU

Kocha wa Kariobangi Sharks, William Muluya, anakabiliwa na mtihani mkubwa watakapomenyana na AFC Leopards katika uwanja wa Nyayo Jumapili huku hatima ya kusalia ligi ikiwa hatarini.

Tofauti ya malengo inaonekana wazi, ambapo AFC Leopards wako nafasi ya pili wakiwa na alama 56 huku Sharks wakiwa nafasi ya 14 na alama 25, alama nne pekee juu ya eneo la kushuka daraja, ingawa mechi hiyo ina mvuto wa kipekee kutokana na baadhi ya wachezaji wa Leopards kuwahi kuchezea Sharks.

Wakati Leopards wakisaka kupunguza pengo dhidi ya vinara Gor Mahia, kwa upande wa Sharks lengo kuu ni kukusanya alama za kutosha ili kujihakikishia kusalia katika ligi kuu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KARIOBANGI SHARKS WAKABILIWA NA MTIHANI MGUMU

OSAMA AHAMIA KLABU YA SWEDEN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *